Saturday, November 27, 2010
Friday, December 11, 2009
SHEREHE ZA UHURU TANZANIA ZAFANA
Sherehe za miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar zafana. Picha ya juu ni Rais Jakaya Kikwete na mkuu majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa sherehe hizo, na picha ya chini ni kikundi cha sanaa toka Uganda kikitumbuza katika sherehe hizo
Sherehe za miaka 48 ya Uhuru wa Tanganyika zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar zafana. Picha ya juu ni Rais Jakaya Kikwete na mkuu majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange wakati wa sherehe hizo, na picha ya chini ni kikundi cha sanaa toka Uganda kikitumbuza katika sherehe hizo
Atinga Ikulu kumpongeza JK
KIJANA Mussa Doto mkazi wa Kata ya Kasamwa, Geita, jana amejikuta akitimiza azma yake ya kutinga Ikulu kwa kutumia usafiri wa baiskeli akitokea Geita kwa lengo la kuja kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Tanzania kwa awa
Dotto alipokelewa jana asubuhi, na Rais Kikwete akitokea Geita hadi kufika Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wake wa baiskeli hadi Ikulu.
Rais Kikwete alimpokea kijana huyo aoliyeonekana kuwa na moyona yeye na kumkaribisha na kumpongeza kijana huyo kwa kuonyehsa ushupavu wake na dhamira yake juu ya yake.
Pia Rais Kikwete mbali na kumshukuru kijana huyo, pia alimuahidi kumsaidia kijana huyo zaidi katika shughuli zake za kilimo ili apate manufaa na mafanikio zaidi
UDSM yaunga mkono kusudio la JK
Fredy Azzah
SIKU moja baada ya Rais Jakaya Kikwete, kueleza kusudio la serikali yake la kuunda tume huru ya kupitia upya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), baadhi ya wahadhiri na viongizi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wameunga mkono uamuzi huo huku wakitaja maeneo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa.
Wakizungumza na Mwananchi jijini Dar es Saal jana, walilitaja mambo makubwa yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kuondoa matatizo ya mikopo kwa wanafunzi kuwa ni pamoja na utendaji wa HESLB.
Mambo mengine ni pamoja kutafuta njia sahihi ya kufanya utambuzi wa uwezo wa mwanafunzi, ili aweze kupewa mkopo unaolingana na hali yake ya maisha.
Pia baadhi ha waadhiri na wanafunzi hao, walisema bodi ya mikopo inapaswa iwe na ofisi huru katika kila kanda au katika mikoa yote.
Hali kadhalika, walishauri idadi ya watumishi wa bodi hiyo, iongezwe kulingana na mahitaji ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu kila mwaka.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mikopo wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Silvanus Joseph, alisema kigezo cha kuangalia mtu kasoma shule gani bila kujua aliyemsomesha kipaswa kutumika katika kutambua uwezo wa mwanafunzi.
Aliongeza kuwa, tume hiyo itapaswa kuongeza fedha ambazo zimekuwa zikitoa kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo na pia kutatua tatizo la ucheleweshwaji wa fedha hizo.
"Lakini tunapata shida kuamini kama haya aliyosema Rais yatatekelezwa kweli, mwaka 2007 alisema hakuna mtoto atakayekosa elimu ya juu kwa sababu ya umasikini wake, lakini tumeshuhudia masikini hao wakikosa nafasi hiyo," alisema.
Alisema mapema mwaka huu, Rais Kikwete alisema fedha za bodi zitaanza kutoka moja kwa moja hazina, ili kuepuka ucheleweshwaji, lakini nalo halikutekelezwa.
Wakati akifungua Maadhimisho ya miaka 50 ya chuo hicho, Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi kushirikiana na viongozi wengine kuhakikisha kuwa tume hiyo inaundwa na mapendekezo yake kutumika katika kuboresha utendaji wa HESLB.
Muhadhiri wa Chuo hicho Profesa Yunus Mgaya, alisema, alisema bodi inapaswa ilipe karo yote kwa wanafunzi
Kero ya mikopo kwa wanafunzi kumalizwa!!!
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu vilivyopo Dodoma. Wanafunzi hao waliandamana kumuunga mkono kuchukua fomu kugombea nafasi ya urais wa Tanzania. (Picha na Freddy Maro).
Na Mwandishi wetu.
FEDHA za kukopesha wanafunzi wa elimu ya juu kwa mwaka ujao wa fedha unaoanzia Julai mwaka huu, zitatengwa maalumu ili zipatikane wakati zinapohitajika na kukomesha uchelewaji wa fedha hizo.
Aidha, mwakani serikali inajipanga kuja na mkakati mwingine mahususi ambao wanafunzi wanaotaka kukopa, watakopeshwa na kujiwekea deni bila kujali uwezo wa wazazi wao.
Rais Jakaya Kikwete alisema hayo jana mjini hapa baada ya risala la wanafunzi wa elimu ya juu wa Mkoa wa Dodoma, kusisitiza matatizo wanayopata wanafunzi hao katika upatikanaji wa mikopo hiyo.
Katika risala hiyo, iliyosomwa na mmoja wa wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Egla Mamoto, wanafunzi hao pamoja na kumpongeza Kikwete kwa wazo lake la kujenga chuo hicho, lakini walisisitiza tatizo la kupata mikopo elimu ya juu.
“Tuko katika mtihani, lakini kwa kuzingatia kuwa wewe ndiyo chimbuko la elimu yetu, tumetenga muda kuja hapa,” alisema Mamoto na kushangiliwa.
“Maandamano haya ni kielelezo cha mapenzi yetu kwako na tunaunga mkono uwe mgombea pekee 2010 na tunazo sababu,” alisema.
Alitaja miongoni mwa sababu hizo kuwa ni utekelezaji makini wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2005 hasa katika elimu ambayo imewagusa na kusimamia wazo lake la ujenzi wa UDOM.
“Ulitoa wazo, ukalisimamia, ukajenga chuo kikuu, kwa hili usiseme wacha sisi wenyewe tunaonufaika tukusemee. UDOM ina hadhi ya kimataifa, je kama si wazo lako, leo hii tungekuwa wapi?” Alihoji mwanafunzi huyo na kushangiliwa na wenzake.
Alisisitiza pamoja na mafanikio hayo wanafunzi wanapata matatizo ya kupata mikopo.
Akijibu hoja hiyo ya mikopo pamoja na nyingine zilizoainishwa katika risala hiyo, Rais Kikwete alisema nia ya kuanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilikuwa njema na wataiendeleza.
Alisema tatizo la kuchelewa kwa fedha za mikopo lilitokana na fedha hizo kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kabla ya kufika HESLB.
Kutokana na tatizo hilo, ambalo wakati mwingine wizara hiyo ilizitumia fedha hizo, sasa kutaundwa mfumo ambao fedha za mikopo hazitapitia wizarani, badala yake zitawekwa maalumu ziwe tayari kwa matumizi ya wanafunzi wakati wowote.
Mbali na mfumo huo, mwakani kutaundwa mkakati wa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 700 kwa wadaiwa vyuo vikuu, ili wanafunzi wa elimu ya juu watakaohitaji mikopo, wapatiwe bila kujali uwezo wa wazazi.
Kuhusu ujenzi wa UDOM, Rais Kikwete alikiri kuwa ujenzi wa chuo hicho haukuwa katika Ilani ya CCM ya 2005, bali waliibadilisha ili kuanza ujenzi wa chuo hicho.
Alifafanua kuwa “katika Ilani imendikwa tutapanua elimu ya juu, lakini wao wakabadilisha kidogo na kuweka, tutajenga chuo kikuu.”
Kauli hiyo ya Rais, imekubaliana na hoja ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, aliyoitoa wiki iliyopita kwamba UDOM haiko katika Ilani ya CCM
Friday, November 19, 2010
Kikwete awatema hawa!
KATIKA baraza lake jipya la mawaziri alilolotangaza jana, Rais Kikwete amewacha baadhi wa mawaziri aliokuwa nao katika awamu yake ya kwanza ya uongozi na kubadili baraza hilo katika sura mpya.
Kikwete amemuacha aliyekuwa Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, aliyekuwa Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Peter Msola, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu a Rais Muungano, Mohamed Seif Khatib.
Wengine aliyekuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Profesa David Mwakyusa, aliyekuwa Waziri wa Aradhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Chiligati.
Waliokuwa manaibu waziri katika wizara mbalimbali waliotemwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Maua Daftari, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Miundombinu, Ezekiah Chibulunje.
Wengine waliopoteza nafasi zao baada ya kushindwa katika uchaguzi mkuu kukosa ubunge ni aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Burian, aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Sera, Uratibu na Bunge, Philip Marmo , aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Aisha Kigoda, na aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza .
Wengine waliopoteza nafai zao ni aliyekuwa Waziri wa Mambo ya NDani ya Nchi, Lawrence Masha, aliyekwua Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera , aliyekuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Magreth Sitta.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi , Dk. James Wanyancha, na aliyekuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala.
Hao ndio waliopoteza nafasi zao katika baraza hili jipya la mawaziri lililotangazwa jana, majaira ya saa 6 mchana, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Na Rais jana alionekana kuwaacha wanahabari hoi mara baaada ya kumaliza kutaja majina wa mawaziri hao alitoa shukrani na kuinuka na kukataa kuulizwa maswali na kuacha wanahabari wakiwa katika butwaa
Kikwete atangaza baraza la mawaziri
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ametangaza baraza lake jipya la mawaziri kukamilisha uundaji wa serikali tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba.
Kikwete amewaacha mawaziri kadhaa wa zamani na kuteua sura mpya kama vile Profesa Anna Tibaijuka.
Rais Kikwete alitaja serikali yake mbele ya waandishi wa habari katika shughuli iliyofanyika Ikulu mjini Dar Es Salaam, akibainisha kuwa hakuna mabadiliko makubwa katika idadi ya wizara, zipo jumla ya wizara 26.
Sura mpya kadhaa zimetajwa ikiwa ni pamoja na Profesa Anna Tibaijuka atakayesimamia wizara ya ardhi na makazi.Profesa Tibaijuka alikuwa mkurugunzi mkuu wa shirika la makazi la Umoja wa Mataifa kabla ya kujiuzulu na kwenda kugombania ubunge jimbo la Muleba Kusini.
Waziri aliyetajwa kinyume na maelezo ya wachambuzi wengi wa kisiasa ni Samuel Sitta, baada ya kuondolewa kiti cha spika wa bunge la Muungano, sasa anakuwa Waziri wa maswala ya Afrika Mashariki.
Mawaziri wengi wa serikali iliyopitwa wamerejeshwa tena katika majukumu waliyokuwa nayo awali kama vile Bernard Membe atakayeendelea kusimamia mambo ya nje.Mustapha Mkullo anarudi kuongoza wizara ya fedha.
Marekebisho kadhaa ameyataja Rais Kikwete katika uundaji wa baraza lake kuwa idara ya vijana imeondolewa kutoka wizara ya kazi na kuhamishiwa wizara ya habari na michezo.
Wanasiasa kadhaa waliokuwa katika serikali iliyopita wameachwa, baadhi yao ni wasomi maarufu kama Profesa Peter Msola aliyekuwa Sayansi na Teknolojia, Profesa Juma Kapuya aliyekuwa Kazi na Profesa David Mwakyusa aliyekuwa afya, mwingine ni kada wa chama kama John Chiligati aliyeachwa wizara ya ardhi.
Waziri hao wataapishwa siku ya Jumamosi katika viwanja vya Ikulu ya Dar Es Salaam.
Orodha kamili ya mawaziri na manaibu waziri hii hapa chini.
Namba
Ofisi/Wizara
Waziri
Naibu Waziri
1.
Ofisi ya Rais
1. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Utawala Bora
Mathias Chikawe
2. Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu
Stephen Wassira
2.
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Hawa Ghasia
3.
Ofisi ya Makamu wa Rais
1. Muungano
Samia Suluhu
2. Mazingira
Dr. Terezya Luoga Hovisa
4.
Ofisi ya Waziri Mkuu
1. Sera, Uratibu na Bunge
William Lukuvi
2.Uwekezaji na Uwezeshaji
Dr. Mary Nagu
5.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
George Mkuchika
1.Aggrey Mwanri
2. Kassim Majaliwa
6.
Wizara ya Fedha
Mustapha Mkulo
1. Gregory Teu
2. Pereira Ame Silima
7.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Shamsi Vuai Nahodha
Khamis Kagasheki
8.
Wizara ya Katiba na Sheria
Celina Kombani
9.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Bernard Membe
Mahadhi Juma Mahadhi
10.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Dr. Hussein Mwinyi
11.
Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. Mathayo David Mathayo
Benedict Ole Nangoro
12.
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Charles Kitwanga
13.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna Tibaijuka
Goodluck Ole Madeye
14.
Wizara ya Maliasili na Utalii
Ezekiel Maige
15.
Wizara ya Nishati na Madini
William Ngeleja
Adam Kigoma Malima
16.
Wizara ya Ujenzi
Dr. John Magufuli
Dr. Harrison Mwakyembe
17.
Wizara ya Uchukuzi
Omari Nundu
Athumani Mfutakamba
18.
Wizara ya Viwanda na Biashara
Dr. Cyril Chami
Lazaro Nyalandu
19.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru Kawambwa
Philipo Mulugo
20.
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Haji Hussein Mpanda
Dr. Lucy Nkya
21.
Wizara ya Kazi na Ajira
Gaudensia Kabaka
Makongoro Mahanga
22.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Sophia Simba
Umi Ali Mwalimu
23.
Wizara ya Habari, Vijana na Michezo
Emmanuel Nchimbi
Dr. Fenella Mukangara
24.
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Samuel Sitta
Dr. Abdallah Juma Abdallah
25.
Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika
Prof. Jumanne Maghembe
Christopher Chiza
26.
Wizara ya Maji
Prof. Mark Mwandosya
Eng. Gerson Lwinge
Pinda aapishwa
RAIS Jakaya Kikwete jana amemwapisha Mbunge wa Katavi [CCM], Mizengo Peter Pinda, kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hafla iliyofanyika katika ikulu ndogo Chamwino Dodoma.
.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka serikali, pamoja na wale wa vyama vya siasa na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini.
Pia katika sherehe hizo wabunge kutoka Chadema hawakuwepo kwenye hafla hiyo.
Pia Rais Kikwete alitoa ahadi ya kuchagua mawaziri waadilifu na wachapakazi atakaoweza kushirikiana nao vizuri katika kipindi hiki cha miaka mitano ijayo.
Mara baada ya kumalizika kwa shughuli hizo, pia alihutubia bunge la 10 na bunge hilo jana liliahirishwa hadi Februari mwakani litakapoanza rasmi
Saturday, November 6, 2010
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Tanzania
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Tanzania uliofanyika siku ya Jumapili.
Bw Kikwete amepata jumla ya kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote zilizopigwa.
Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dr Wilbrod Slaa yuko nafasi ya pili kwa kura milioni mbili na laki mbili, sawa na asilimia 26.34.
Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, ameambulia nafasi ya tatu baada ya kukusanya kura 695,668 ambazo ni mgao wa asilimia nane.
Wagombea wengine na asilimia ya kura zao ni kama ifuatavyo Peter Mziray, asilimia 1.12.
Hashim Rungwe asilimia 0.31, Mutamwega Mgahywa asilimia 0.20 na Fahmi Dovutwa asilimia 0.15.
Bw Kikwete ataapishwa kesho kutumikia awamu ya pili kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Tanzania uliofanyika siku ya Jumapili.
Bw Kikwete amepata jumla ya kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote zilizopigwa.
Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dr Wilbrod Slaa yuko nafasi ya pili kwa kura milioni mbili na laki mbili, sawa na asilimia 26.34.
Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, ameambulia nafasi ya tatu baada ya kukusanya kura 695,668 ambazo ni mgao wa asilimia nane.
Wagombea wengine na asilimia ya kura zao ni kama ifuatavyo Peter Mziray, asilimia 1.12.
Hashim Rungwe asilimia 0.31, Mutamwega Mgahywa asilimia 0.20 na Fahmi Dovutwa asilimia 0.15.
Bw Kikwete ataapishwa kesho kutumikia awamu ya pili kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
JK. Aibuka mshindi wa urais
Jakaya Kikwete, Mgombea wa urais wa CCM ambaye alitangazwa jana kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuzoa asilimia 61.17 ya kura, ataapishwa leo jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa Uhuru.
Maandalizi ya sherehe ya kumuapisha rais mpya wa Tanzania yamepamba moto kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Jakaya Mrisho Kikwete alitangazwa rasmi jana kuwa ndiye rais mpya wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo baada kushinda uchaguzi wa urais kwa kuzoa jumla ya kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17.
Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dr Wilbrod Slaa alishika nafasi ya pili kwa kujikusanyia kura 2.2 sawa na asilimia 26.34 ya kura zote zilizopigwa.
Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF alipata kura 695,668 sawa na asilimia 8 wakati mgombea wa NCCR Mageuzi alijinyakulia kura 26,308, mgombea wa TLP kura 17,482 na nafasi ya mwisho imekwenda kwa UPDP kura 13,176.
Sherehe ya kumuapisha Kikwete kuwa rais itafanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku vikundi mbalimbali vya burudani vikiwa tayari kutoa burudani wakati wa sherehe hizo.
Tangua juzi na jana vikundi mbalimbali vya ngoma za asili na vikundi
vya jeshi vilikuwa katika mazoezi makali kwaajili ya sherehe hizo.
Mzoezi hayo yaliyokuwa yakiratibiwa na usalama wa taifa yalionekana
kupamba moto kwa kuvishirikisha vyombo vya habari ikiwa ni kupewa
maelekezo namna watakavyojipanga kupiga picha na ratiba kamili.
Vikundi vya ngoma vilivyohusika ni pamoja na kundi la THT Tanzania
House of Talent, kikundi cha mkoa wa Ruvuma na cha Zanzibar.
Katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa tayari waandishi wa
habari wamepewa vitambulisho maalumu tofauti na vya uchaguzi.
Gonga linki chini kwa picha za Jakaya Kikwete kutangazwa rasmi kuwa rais pamoja na picha za maandalizi ya kuapishwa kwake kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo
Friday, November 5, 2010
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Tanzania uliofanyika siku ya
Mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa Tanzania uliofanyika siku ya Jumapili.
Bw Kikwete amepata jumla ya kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17 ya kura zote zilizopigwa.
Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dr Wilbrod Slaa yuko nafasi ya pili kwa kura milioni mbili na laki mbili, sawa na asilimia 26.34.
Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, ameambulia nafasi ya tatu baada ya kukusanya kura 695,668 ambazo ni mgao wa asilimia nane.
Wagombea wengine na asilimia ya kura zao ni kama ifuatavyo Peter Mziray, asilimia 1.12.
Hashim Rungwe asilimia 0.31, Mutamwega Mgahywa asilimia 0.20 na Fahmi Dovutwa asilimia 0.15.
Bw Kikwete ataapishwa kesho kutumikia awamu ya pili kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Subscribe to:
Posts (Atom)