No Pain No Gain Maishani

Saturday, November 6, 2010

JK. Aibuka mshindi wa urais



Jakaya Kikwete, Mgombea wa urais wa CCM ambaye alitangazwa jana kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuzoa asilimia 61.17 ya kura, ataapishwa leo jijini Dar es Salaam kwenye uwanja wa Uhuru.
Maandalizi ya sherehe ya kumuapisha rais mpya wa Tanzania yamepamba moto kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Jakaya Mrisho Kikwete alitangazwa rasmi jana kuwa ndiye rais mpya wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo baada kushinda uchaguzi wa urais kwa kuzoa jumla ya kura 5,276,827 ambazo ni sawa na asilimia 61.17.

Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dr Wilbrod Slaa alishika nafasi ya pili kwa kujikusanyia kura 2.2 sawa na asilimia 26.34 ya kura zote zilizopigwa.

Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF alipata kura 695,668 sawa na asilimia 8 wakati mgombea wa NCCR Mageuzi alijinyakulia kura 26,308, mgombea wa TLP kura 17,482 na nafasi ya mwisho imekwenda kwa UPDP kura 13,176.

Sherehe ya kumuapisha Kikwete kuwa rais itafanyika leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku vikundi mbalimbali vya burudani vikiwa tayari kutoa burudani wakati wa sherehe hizo.

Tangua juzi na jana vikundi mbalimbali vya ngoma za asili na vikundi
vya jeshi vilikuwa katika mazoezi makali kwaajili ya sherehe hizo.

Mzoezi hayo yaliyokuwa yakiratibiwa na usalama wa taifa yalionekana
kupamba moto kwa kuvishirikisha vyombo vya habari ikiwa ni kupewa
maelekezo namna watakavyojipanga kupiga picha na ratiba kamili.

Vikundi vya ngoma vilivyohusika ni pamoja na kundi la THT Tanzania
House of Talent, kikundi cha mkoa wa Ruvuma na cha Zanzibar.

Katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa tayari waandishi wa
habari wamepewa vitambulisho maalumu tofauti na vya uchaguzi.

Gonga linki chini kwa picha za Jakaya Kikwete kutangazwa rasmi kuwa rais pamoja na picha za maandalizi ya kuapishwa kwake kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka mitano ijayo

No comments:

Post a Comment