No Pain No Gain Maishani

Friday, November 19, 2010

Pinda aapishwa


RAIS Jakaya Kikwete jana amemwapisha Mbunge wa Katavi [CCM], Mizengo Peter Pinda, kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hafla iliyofanyika katika ikulu ndogo Chamwino Dodoma.
.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka serikali, pamoja na wale wa vyama vya siasa na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini.

Pia katika sherehe hizo wabunge kutoka Chadema hawakuwepo kwenye hafla hiyo.

Pia Rais Kikwete alitoa ahadi ya kuchagua mawaziri waadilifu na wachapakazi atakaoweza kushirikiana nao vizuri katika kipindi hiki cha miaka mitano ijayo.

Mara baada ya kumalizika kwa shughuli hizo, pia alihutubia bunge la 10 na bunge hilo jana liliahirishwa hadi Februari mwakani litakapoanza rasmi

No comments:

Post a Comment