No Pain No Gain Maishani

Saturday, December 11, 2010

Sherehe za uhuru zafana wengi wajitokeza


SHEREHE za kuadhimisha miaka 49 ya uhuru zilizofanyika katkka uwanja wa Uhuru Dar es Salaam zilifana kwa wakazi wengi wa jiji kujitokeza katika sherehe hizo.

Maelfu ya Wakazi hao waliongozwa na Rais Jakaya Kikwete ambapo alikagua magwaride na kusherehesha sherehe hizo.

Sherehe hizo zilishereheshwa na ndege za kijeshi kutoka Ngerengere pamoja magwaaride ya jeshi mbalimbali na vijana wa halaiki kupamba sherehe hizo kwa kuimba wimbo wa taifa.

Katika sherehe hizo Viongozi kutoka kada mbalimbali kutoka serikali na viongozi wa dini walihudhuria sherehe hizo wakiwemo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi , Maalim Seif Sharif Hamad, wakiwemo na marais wastaafu na wengine wengi .

Rais Jakaya Kikwete mara bada ya kufika uwanjani hapo aliweza kupigiwa mizinga ipatayo 21 na kisha kukagua gwaride na vijana wa halaiki wapatao zaidi ya 1000 kutoka shule za msingi waliweza kuonyehsa ufundi kwa kujipanga na kutoka neno uhuru.

Tanzania imetimiza miaka 49 toka kupata kwa uhuru wake kutoka kwa Muingereza Desemba 9, 1961

No comments:

Post a Comment