Monday, October 4, 2010
HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, DODOMA , 12 JUNI, 2006
HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS
WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE
UFUNGUZI WA JENGO LA UKUMBI MPYA WA BUNGE,
DODOMA , 12 JUNI, 2006
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania;
Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein;
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid
Karume;
Waziri Mkuu, Mhe. Edward Lowassa
Mheshimiwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,
Mhe. Pandu Ameir Kificho;
Waheshimiwa Maspika Waalikwa;
Waheshimiwa Mawaziri;
Waheshimiwa Wabunge;
Waheshimiwa Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana.
Niruhusuni niungane nanyi kumshukuru Mwenyezi Mungu
kwa kutufikisha salama siku ya leo kutukutanisha pamoja hapa siku
ya leo kushuhudia ufunguzi wa Jengo Jipya la Ukumbi wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunialika kushiriki
kwenye shughuli hii. Mmenipa heshima kubwa kwa kunishirikisha
kwenye tukio hili la kihistoria. Nawashukuru kwa mapokezi mazuri.
Naomba pia nitumie fursa hii na mimi kuongeza kauli ya
kuwakaribisha wageni wetu kutoka nje ya nchi. Nafurahi kwamba
2
2
mmeweza kujumuika nasi, jambo ambalo linaasharia ukaribu na
udugu uliopo baina ya nchi zetu na watu wake.
Mheshimiwa Spika,
Mnamo mwezi wa Februari, 2005 tulikuwa hapa, tukiongozwa
na Mhe. Frederick Sumaye, Waziri Mkuu wa wakati ule kwa ajili ya
kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Jengo hili. Kazi hiyo sasa
imekamilika hiyo sasa imekamilika na ushahidi ni jengo hili
linalopendeza lililoko mbele yetu na sherehe ya leo.
Nafarijika sana kuungana nanyi leo, takriban miezi kumi na
saba baadaye, katika sherehe za ufunguzi wa jengo jipya la Bunge.
Sherehe ambayo imefana sana. Kuanzia kesho Waheshimiwa
Wabunge mtaanza kulitumia mnapoanza Mkutano wa Bunge la
Bajeti. Hongereni.
Nawapongeza wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine
kufanikisha ujenzi wa ukumbi huu. Nawapongeza sana kwa kazi hii
kubwa na nzuri. Hususan, napenda kumtambua Spika Mstaafu,
Mzee wetu Pius Msekwa kwa kubuni wazo la kuwa na jengo hili na
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Frederick Sumaye kwa uwezeshaji wa
utekelezaji.
Pongezi mahsusi nazitoa kwa Serikali yetu ya Awamu ya Tatu
kwa kuridhia wazo la ujenzi wa ukumbi huu na kusimamia
maandalizi yote muhimu ya ujenzi wake. Pongezi maalum
zimuendee Rais Mstaafu, Mhe. Benjamin Mkapa kwa kukubali wazo
3
3
la kujengwa jengo hili na kuafiki utaratibu mzima wa kupata fedha
za ujenzi. Uamuzi wake huo ndio uliowezesha kuwepo kwa jengo
hili tunalojivunia nalo. Nafurahi kwamba umepata nafasi ya kuja
kushuhudia matunda ya kazi yako nzuri.
Napenda pia kukushukuru wewe binafsi, Mheshimiwa Spika,
pamoja na Waziri Mkuu, Mhe. Edward Lowassa kwa uongozi wenu
mahiri uliowezesha ujenzi kukamilika kwa wakati muafaka.
Mheshimiwa Spika;
Pongezi na shukrani pia nazitoa kwa Katibu wa Bunge na timu
yake, Waziri wa Fedha na Viongozi wengine wa Serikali kwa
kushirikiana vyema kwa kushirikiana vyema katika kuhakikisha kazi
hii inakamilika kwa ufanisi mkubwa.
Vilevile, shukrani ziende kwa wajenzi wa jengo hili kwa kazi
nzuri na kwa Mashirika ya Mifuko ya Pensheni kwa pamoja kukubali
kufadhili na kusimamia ujenzi wa ukumbi huu. Mashirika haya ni
Public Service Provident Fund (PSPF), Local Authority Provident
Fund (LAPF), Parastatals Provident Fund (PPF) na National Social
Security Fund (NSSF). Nawapongeza kwa kuwekeza kwenye mradi
huu ambao ni fahari na heshima kubwa kwa Taifa.
Sisi katika Serikali tunatambua wajibu wetu wa kuwalipa kwa
gharama kubwa mlioingia. Tunawaahidi tutafanya hivyo kama
tulivyokubaliana. Mimi na wenzangu Serikalini tunajua kuwa
4
4
mmetumia fedha za wanachama wenu ambazo hazina budi walipwe
wakati ukifika. Hatutawaangusha.
Mheshimiwa Spika, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana
Kujenga ukumbi wa Bunge wenye kukidhi mahitaji ya Bunge
letu na hasa kwa mujibu wa mahitaji na mazingira ya karne ya 21 ni
changamoto ya aina yake. Lakini, kwa niliyoyaona ndani ya jengo
hili changamoto hiyo imejibiwa kwa ukamilifu. Kwa kila hali jengo
hili linafanana kabisa na Bunge la wakati tulionao sasa.
Jengo jipya tunalolizindua leo litaliwezesha Bunge letu sasa
kuwa na vifaa vipya vya shughuli za kibunge tena vilivyotengenezwa
kwa teknolojia ya kisasa. Ukumbi huu utawawezesha Waheshimiwa
Wabunge wetu kupata huduma bora na hivyo kufanya shughuli za
uwakilishi kwa ufanisi wa kiwango cha juu. Ni ukumbi wenye hadhi
ya kimataifa unaowapa Wabunge vionjo vya Bunge katika karne ya
21.
Mheshimiwa Spika;
Kinachonipa faraja zaidi ni kwamba ukumbi huu mpya, tofauti
na kumbi zote zilizowahi kutumika kwa shughuli za Bunge huko
nyuma, unatoa fursa zaidi kwa wananchi walio wengi zaidi kufuatilia
mijadala ya Bunge kwa karibu zaidi.
5
5
Kwa kuwezesha ushiriki mpana zaidi wa wananchi kwenye
shughuli za Bunge, jengo hili sasa linatuwezesha kupiga hatua kubwa
zaidi katika kujenga na kuimarisha demokrasia nchini.
Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge
Nilipata kusoma pahala kwamba, wakati jengo la Bunge la
Uingereza (The House of Commons) linajengwa upya baada ya
kubomolewa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Winston Churchil
alisema “we shape our buildings, and they shape us”.
Sina shaka akilini mwangu kuwa, kwa hakika jengo hili litabadilisha
namna tunavyofanya kazi ikiwa ni pamoja na mienendo na mitazamo
yetu kuhusu vikao na maamuzi ya Bunge. Ni matumaini yangu
kwamba jengo hili litatubadilisha kwa kutujengea ufahari wa kuwa
na mahali pazuri na penye heshima pa kufanyia kazi.
Mheshimiwa Spika,
Kwa ninavyoelewa mimi, jukumu la msingi la Mbunge ni
kuyapa sauti matumaini, matarajio, na matakwa ya watu wetu.
Wabunge ni vipaza sauti (megaphones) vya Watanzania
waliowachagua.
Bila ya shaka kwa kuutumia kwa ukamilifu ukumbi huu wa
Bunge ulio mzuri na wenye vifaa vya kisasa, sauti za Watanzania
zitasikika bila mikwaruzo. Aidha, matakwa na matarajio yao
6
6
yatawasilishwa, kujadiliwa, kufanyiwa kazi na kupatiwa majibu kwa
ufanisi zaidi sasa.
Ndugu zangu, leo tumepata Jengo la Bunge jipya, zuri na la
kisasa. Tena, ni jengo la kwanza katika historia ya nchi yetu ambalo
limejengwa kwa uamuzi wa Bunge na kwa mujibu wa matakwa
yake. Bahati nzuri tunalo Bunge lililokomaa kama taasisi na tunao
Wabunge waliopevuka kama watetezi halali wa maslahi ya
Watanzania waliowachagua. Sasa kazi kwenu.
Vile vile, napata faraja kubwa kwamba tunalo Bunge makini,
lenye Wabunge wa mchanganyiko muafaka kwa maana ya vyama,
taaluma, fani, jinsia, umri na rika. Nawapongeza Waheshimiwa
Wabunge na uongozi wa Bunge kwa juhudi mnazoendelea nazo za
kuimarisha taratibu na kanuni mbalimbali za utawala na uendeshaji
wa Bunge ili kuongeza ufanisi katika taasisi yetu hii muhimu.
Ni imani yangu kwamba, kwa kuwawekea mazingira mazuri ya
kufanyia kazi, ikiwa ni pamoja na kuwa na mahali penye hadhi na
heshima pa kukutania kama hapa, nafasi na mchango wa Wabunge
kwa maendeleo ya Taifa letu utakuwa mkubwa zaidi.
Mheshimiwa Spika;
Serikali kwa upande wake, itaendelea kuchangia juhudi za
kuboresha mazingira ya kufanyia kazi zenu hapa Bungeni na
Majimboni. Tutafanya kila kinachowezekana, kulingana na uwezo
7
7
uliopo, kuwapatia mahitaji ya kuwawezesha kuwa Wabunge wazuri
kwa wapiga kura wenu.
Hata hivyo, naomba mtuelewe kwamba pale tutakaposhindwa
kutimiza yote mnayoyahitaji si kwa sababu ya kupuuza umuhimu wa
Bunge bali ni kwa sababu ya kukwazwa na uwezo wa rasilimali.
Mahitaji ni mengi, wahitaji ni wengi lakini uwezo una ukomo.
Kuwepo kwa jengo hili ni ushahidi tosha kuwa tunajali.
Mheshimiwa Spika;
Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Bunge, kama mhimili
huru wa utawala wa nchi yetu. Wote tuna mteja mmoja: Mwananchi
wa Tanzania. Ili tumtumikie vizuri na tukidhi matarajio yake, suala la
kushirikiana baina yetu halina mbadala na wala halina mjadala. Katu
tusifanye kinyume chake. Mimi siamini kwamba ufanisi wa Mbunge
unapimwa kwa umahiri wa kupinga hoja za Serikali. Na siamini pia
kwamba Serikali makini nayo ni ile ambayo wakati wote inaziba
masikio yake kwa maoni na mawazo ya Wabunge. Nawaahidi
ushirikiano wangu binafsi na wa wenzangu wote Serikalini.
Mheshimiwa Spika, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Jengo hili, si tu kwamba linapendezesha sura ya Mji wa
Dodoma, bali pia linaipa haiba mpya demokrasia yetu. Hiki ni kiota
cha mijadala muhimu ya kitaifa, mijadala itakayoamua mwelekeo wa
8
8
demokrasia yetu, hatma ya maendeleo yetu na mustakabali wa Taifa
letu. Leo tunafungua ukumbi wa wananchi kwa kuwa mawazo,
maoni na mashauriano juu ya masuala yanayowahusu wao ndimo
humu yatakapokuwa yakijadiliwa na kutolewa maamuzi.
Mheshimiwa Spika, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana,
Wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la Bunge la Scotland,
Oktoba mwaka wa juzi, Edwin Morgan, Mshairi wa Taifa (national
poet) wa Scotland aliandika shairi mahsusi, ambalo napenda
kunukuu sehemu yake.
“We give you our consent to govern, don’t pocket it and ride away.
We give you our deepest dearest wish to govern well, don’t say we
have no mandate to be so bold.
We give you this great building, don’t let your work and hope be
other than great when you enter and begin.
So now begin. Open the doors and begin”
Tafsiri:
Tumewapa ridhaa ya kutawala, msiitie mfukoni na kukimbia nayo;
Tunawatakia heri nyingi na mapenzi ya dhati mtawale vyema,
msiseme hamkuwa na mamlaka ya kuwa shupavu;
Tunawapa jengo hili kubwa, msiruhusu kazi na matumaini yenu nayo
yasiwe makubwa mtakapoingia ndani na kuanza;
Sasa anzeni kazi. Fungueni milango na muanze;
9
9
Mheshimiwa Spika;
Ulinialika kuja kufungua rasmi jengo jipya la Bunge letu
tukufu. Kwa kukata utepe, nilitimiza wajibu huo. Kwa heshima na
taadhima kubwa naomba niseme kuwa sasa Ruksa! Fungueni
milango muingie ndani na muanze kazi.
Nawatakia kila la heri.
Ahsanteni kwa kunisikilliza!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment