No Pain No Gain Maishani

Saturday, October 2, 2010

JK atetea safari za nje




RAIS Jakaya Kikwete, amelaani na kushangazwa na watu wanaomshangaa kwa kusafiri mara kwa mara kwenda nje ya nchi na kusema safari hizo zina maana kubwa na kusema huenda safari hizo zisingekuwepo watanzania walio wengi wangekufa kwa njaa.



Hayo ameyasmea jana katika kampeni zake zinazoendelea mkoani Tabora alipokuwa wilayani Urambo na kukiri kuwa safari hizo zina maana kubwa si kwake tu bali ni kwa watanzania walio wengi zinawanufaisha.




Alisema kuwa safari hizo huwa anaende kuomba misaada kwa wahisani na kunufaisha nchi kama nchi na si yeye kama watu wanavyombeza sasa na kumshangaa.



Kikwete alijitetea kwa kusema kuwa “ Mimi ninapokwenda nje nakwenda kwa malengo, sijiendei tu naomba mtambue, lazima niende huko nikutane na watu mbalimbali watakaoweza kusaidia nchi yetu” alimalizia ka utani na kusema “Siwezi kukaa Ikulu tu kuangalia uzuri wa mke wangu Salma” alisema Jk …



Alihoji ka kusema hivi kama nisingeenda Marekani kuongea na rafiki yangu Bush tungewezaje kusaidia kudhibiti malaria? “nilipokwenda kule nikakutana na rafiki yangu akaniambia nitamaliza tatizo la malaria kwako na kweli akatununulia vyandarua vyenye thamani ya Dola milioni 78,” alisema.




Hivyo aliwataka watanzania anaolalamikia safari zake watambue kuwa yeye anakwenda ka kuitengeneza nchi na kukutana na wahisani na mara nyingi safari zinakuwa za kiserikali

No comments:

Post a Comment