Monday, October 4, 2010
RAIS JAKAYA KIKWETE anataraji kuzuru wilayani KIlosa kesho jumapili kuwafariji wakazi waliokumbwa na mafuriko
RAIS JAKAYA KIKWETE anataraji kuzuru wilayani KIlosa kesho jumapili kuwafariji wakazi waliokumbwa na mafuriko wilayani humo pamoja na kukagua miundombinu iliyo haribiwa na mafuriko hayo yaliyoikumba wilaya hiyo toka desemba 26 mwaka jana
Habari zimeeleza kuwa jk atawasili mkoani Morogoro leo jioni na kesho asubuhi kuelekea kilosa kwa ajili ya kazi hiyo.
Habari zimeeleza kuwa kama hali ya hewa itaruhusu atazuri angani kwa kutumia helkopta kukagua miundombinu hiyo na kama mambo yatakwenda sawa anaweza kwenda kukagua hata mafuriko yaliyotokea wilayani Mpwapwa imeelza taarifa hiyo.
Hata kama amechelewa kuzuru wilayani KIlosa lakini rais alikuwa akifuatilia kwa karibu taarifa za mafuriko hayo na kutoa maelekezo kadhaa ya kuwawezesha wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo kuishi katika hali salama.
Moja ya mambo aliyoyafanya ni pamoja na kumtuma waziri mkuu mizengo pinda wilayani humo pamoja na kutuma vikosi vya jeshi la wananchi jwtz kwenda kujenga makazi ya muda kwa waathirika hususan wanaoishi katika shule za msingi ili kupisha wanafunzi waweze kusoma
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment